ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 26, 2018

WATU WAWILI WAUAWA NA KUTOLEWA VIUNGO GEITA.





Wakazi wawili wa Kijiji cha Lubanga mkoani Geita wameuwawa kwa kukatwa mapanga na kunyofolewa viungo mbalimbali vya mwili, tukio linalodaiwa kufanywa na watu wasiojulikana na kutoweka na viungo hivyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani humo wakati akizungumza na www.eatv.tv , Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki na waliouawa ni mtu na shangazi yake suala ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.

Kamanda Mponjoli amewataja waliouawa kuwa ni Kija Lushanga (70) na Pendo Bukelebe (48) ambapo amesema kuwa imani potofu za kishirikina imekuwa jambo la kawaida kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa na ni changamoto kwa Jeshi la Polisi katika majukumu yake kwani matukio mengi yanafanywa na wanafamilia.

“Kufuatia mauaji hayo jeshi la polisi tumekamata watu wanne kwa mahojiano na uchunguzi bado unaendelea na hatuwezi wataja kutokana na sababu za kiusalama, lakini Kanda ya Ziwa hakuna uelewa wa wananchi kutoamini kuwa imani za kishirikina ni matatizo na wao kujichukulia sheria mkononi”, amesema Mponjoli

Ameongeza kuwa, “Jamii inayozunguka eneo hili inahusisha mauaji haya na imani za kishirikina lakini sisi kama Jeshi la Polisi kwa sasa tunachukulia kuwa ni mauaji isipokuwa tutakapokamilisha uchunguzi ndio tutajua nini kiini cha mauaji na watu kuondoka na viungo hivyo”.

Mkoa wa Geita ni miongoni mwa mikoa yenye matukio ya mauaji ya wanawake kukatwa mapanga kutokana na kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo Mei 17, 2018 Sophia Sitta mkazi wa kijiji cha Mwabasabhi wilayani Chato aliuawa na mwili wake kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.

April 05, 2018 wanawake wanne wilayani Nyang’hwale waliuawa kwa kunyongwa kisha miili yao kutupwa porini. Juni 06 ,2018 polisi walimuua kwa kumpiga risasi Panda Kinasa (36) ambaye alikua akiteka watu kudai fedha kisha kuwaua.

Takwimu za polisi za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa watu 32 walipoteza maisha mkoani Geita kwa kipindi cha miezi mitatu Oktoba Disemba 2015 kutokana na mauji ya kutumia mapanga yanayodaiwa kusababishwa na imani za kishirikina.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.