ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 10, 2016

BREAKING NEWS: TETEMEKO KUBWA LIMEIKUMBA MWANZA, BUKOBA, CHATO NA MUSOMA

 Hali ya taharuki imelikumba leo jiji la Mwanza kwenye majira ya saa 9:40 alasili baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi ambalo liliweza kudumu kwa muda wa dakika kadhaa.

Hali ilikuwa tete kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali ambao either makazi yao au shughuli zao ziko kwenye majengo marefu mjini hapa kwani walilazimika kubanana kwenye milango ya kutokea al-muradi kila mmoja kutaka kuendoka kwenye majengo hayo na jitihada za kujinusuru. 

Mpaka sasa Jembe Fm inaendelea kukusanya taarifa kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza kubaini athari zilizoweza kujitokeza.
KUSIKILIZA KILICHOTOKEA BOFYA PLAY (SAUTI KUKUJIA HIVI PUNDE)














KUTOKA HUKO BUKOBA Nyumba kadhaa zimeanguka mjini manispaa na halmashauri ya Bukoba, baada ya kutokea tetemeko la ardhi ambayo kipimo chake akijaripotiwa, huku taarifa kutoka Misenyi zinasema taharuki imetanda na wakaazi wametoka nje ya nyumba ilhali taarifa za majeruhi na vifo hazijatolewa ingawa tumeshuudia watu wakikimbizwa hospitalini. Tutawaletea undani.
Pia inasemekana Tetemeko hilo limetokea CHATO NA MUSOMA..

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.