Baadhi ya Wadau wa Mifugo mkoani Arusha waliohdhuria kikao cha pamoja na TADB wakitoa maoni yao kuhusiana hali ya hupatikanaji wa mikopo katika kusaidia sekta ya mifugo mkoani humo |

Na mwandishi wetu, Arusha
Wadau
wa sekta ya mifugo mkoani Arusha wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB)
kuwasaidia katika kuendeleza sekta hiyo kwa kuwapatia mikopo na
mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa
ng’ombe wa nyama na maziwa.
Akizungumza
katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Kampuni ya Nyama ya
Arusha, kwa
niaba ya wafugaji wa mkoa wa Arusha, Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Nyama
cha Arusha, Bw. Fabian Kissiagi amesema ukosefu na ufinyu mkubwa wa
upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa
katika sekta ya mifugo inawapa changamoto katika
uendelezaji wa sekta ya mifugo nchini.
Bw. Kissiagi ameongeza ukosefu wa mikopo ya uhakika inarudisha nyuma ukuaji wa sekta ya mifugo
na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.
“Hali
ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo
mingi kutoka
taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa
na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo tunaiomba TADB kutusaidia
kutatua changamoto hii,” alisema.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga
amesema Serikali iliamua
kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia
kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha
upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi
katika
kilimo nchini.
Bw.
Assenga ameongeza kuwa sekta ya mifugo ni mojawapo ya minyororo ya
mwanzo inayopatiwa
mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali
hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama na
maziwa nchini.
Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe
wa Nyama na Maziwa.
“Benki
inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa
mitambo na ufungaji
wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya
kunyweshea na pamoja na usindikaji wa nyama na maziwa kwa ajili ya
kuongeza thamani nyama na maziwa,” alisema Bw. Assenga.
Naye,
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha amesema
kuwa TADB inatoa
mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili
(2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na
Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).
“Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo
kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
Mkoa wa Arusha unashika nafasi ya tatu kati ya mikoa yenye mifugo mingi nchini ambapo inakadiriwa
kuwa na zaidi ya ng’ombe, mbuzi na kondoo milioni tatu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.