ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 11, 2017

MONGELLA ACHARUKA FEDHA ZA ELIMU

NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amekiagiza chama cha Walimu Mkoa wa Mwanza (CWT) kuleta matokeo ya Wakuu wa Shule 28 waliosemekena kutumia fedha ya Elimu bila malipo kinyume cha utaratibu.

Amesema atakayethibitika amekula fedha hizo mara baada ya uchunguzi hawana budi kuondolewa na kwamba hakutakuwa na muda wa kuwavumilia.

Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa Elimu Wilaya ya Nyamagana amesema hakuna  mtu  atakeonewa na atakaethibitika ataondolewa kwenye Ukuu wa shule.

“Jambo hili nimeamua kulisema hapa kwa sababu lina minong,ono mingi kwamba watu wanaonewa hakuna mtu atakaeonewa,kubebwa wala kupendelewa kila mtu apate haki yake inayostahili”amesema Mongella.

Ameeleza kuwa fedha hizo ni moja ya ahadi ya Rais Mgufuli wakati wa kampeni zake na kwamba ni jambo ambalo alilifanya mara baada ya kuingia ofisini ambapo amesema licha ya fedha hizo kufika mashuleni bado hakidhi mahitaji.

“Licha ya kwamba fedha haitoshi lakini tutawezaje kuongezewa nyingine wakati hiyo tulionayo tunakula, leo hii ndugu zangu kuna shule hapa , wakuu wa shule mpo fedha ya shule iliyokuja ya elimu bila malipo wengine mmeshaimaliza hamjakaa hata na kamati za shule, wala bodi ya shule haijui kitu watu tunatakiwa tusome alama ya nyakati”ameeleza Mongella.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.