Katibu
Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto)
akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia)
wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji
mkoani Arusha.
Katibu
Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati)
akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea
Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha. Ugeni
uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega akihimiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na ugeni kutoka
TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis
Assenga (kushoto) akizungumza na Katibu
Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (hayupo pichani)
wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji
mkoani Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw.
Augustino Chacha.
Mkurugenzi
wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (kulia)
akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki
wakati akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard
Kwitega (hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga.
Meneja wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. Geofrey Mtawa (kulia) akitoa takwimu za mahitaji ya mikopo ya mkoa wa
Arusha. Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. George Nyamrunda.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akimkabidhi muhtasari wa maeneo ya uwekezaji Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia).
Na Mwandishi wetu,
Wito umetolewa kwa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuchangamkia fursa
za uwekezaji katika serkta ya kilimo na mifugo kwa kuwapatia mikopo
wakulima wanaojishughulisha katika sekta hizo mkoani Arusha ili
kuchagiza sekta ya kilimo mkoani humo.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB
wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Bw. Kwitega amesema kuwa mkoa wa Arusha una fursa nyingi za uwekezaji hasa katika maeneo ya kilimo na ufugaji.
Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema uanzishwaji
wa TADB unatokana na Serikali
kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya
Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji
wa mikopo na mitaji ya riba nafuu
ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.
Bw. Assenga mkoa wa Arusha utaingizwa
rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na
wafugaji wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa zinazotolewa
na TADB.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.