Timu ya Yanga iliweza kujiandikia bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake Saimoni Msuva katika dakika 38 za mchezo katika kipindi cha kwanza na kuisababisha Kagera Sugar kuanza upya mashambulizi yake na hatimaye yaliweza kuzaa matunda kwa kuweza kusawazisha bao hilo ndani ya dakika 45 (+2) za nyongeza kabla kipindi cha kwanza kuisha kwa kupitia mchezaji wake Mbaraka Yusufu.
Mara tu timu hizo ziliporejea kutoka mapumziko, hali ya mchezo ilionekana ya tofauti kutokana timu zote zikishambuliana kwa nguvu nyingi ili kuhakikisha kupata ushindi lakini bahati ikaangukia kwa Yanga katika dakika 53 za mchezo waliweza kuona nyavu za wapinzani wao kwa mara ya pili kwa kupitia krosi matata kutoka kwa Haruna Niyonzima na kumaliziwa golini na Obrey Chirwa.
Kwa ushindi huo timu ya Yanga kwa sasa ndiyo imekuwa inaongoza ligi kuu kwa pointi 62
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.