Korea Kaskazini imelaani tena jaribio la
kutaka kumuua kiongozi wake ambalo limetekelezwa na mashirika ya
kijasusi ya Marekani na Korea Kusini na kulitaja jaribio hilo kuwa sawa
na tangazo la vita.
Ubalozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa umetoa
taarifa na kusema nchi hiyo itaanza oparesheni dhidi ya magaidi ambao
walihusika na njama ya kutaka kumuua kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.Taarifa hiyo imesema Pyongyang ina azma imara ya kuwasaka bila huruma na kuwaangamiza magaidi wote wa shirika kuu la kijasusi la Marekani CIA na shirika la kijasusi la Korea Kusini waliohusika na njama hiyo.
Taarifa hiyo imetoa wito kwa nchi za Umoja wa Mataifa kuunga mkono jitahada za Korea Kaskazini katika kukabiliana na magaidi hao waliotumwa na CIA.
Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilitoa taarifa na kusema kuwa, CIA na Idara ya Intelijensia ya Korea Kusini zinapanga kutumia silaha ya kemikali kumuua kiongozi wa nchi hiyo.
Haya yanajiri katika hali ambayo, hali ya taharuki ingali imetanda
katika Peninsula ya Korea haswa baada ya Marekani kufanyia majaribio
kombora lake la "Minuteman III" lenye uwezo wa kupiga umbali wa karibu
kilomita elfu sita na 760.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.