Askari 12 wa Kikosi cha Kulinda Amani cha
Umoja wa Mataifa MINUSCA wameuawa na kujeruhiwa baada ya msafara wa
magari yao kutekwa nyara na kushambuliwa na genge la waasi huko Jamhuri
ya Afrika ya Kati.
Stephane Dujarric, Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema
wanajeshi wanne wa UN wameuawa huku wanane wakiachwa na majeraha mabaya,
baada ya kuzuka makabiliano kati yao na kundi la waasi wa Kikristo la
Anti-Balaka, karibu na eneo la Bangassou, yapata kilomita 474 mashariki
mwa mji mkuu, Bangui Jumatatu usiku.Amesema mbali na mauaji na majeraha hayo, askari mmoja wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ametoweka na hatima yake haijulikani hadi sasa.
Wapiganaji wa Kikristo wa Anti-Balaka huko CAR
Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres ametoa taarifa ya kulaani
mashambulizi hayo dhidi ya maafisa wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa,
akisisitiza kuwa kuhujumiwa askari wa umoja huo ni sawa na jinai za
kivita.
Mapigano ya hivi karibuni katika miji ya Bambari, Ouaka, Mkoa wa
Kati na Makoum, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mbali na kuua
makumi ya raia, yamesasabisha maelfu ya raia wa nchi hiyo kukimbilia
nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro, mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano ya kikaumu yaliyopelekea kuondolewa madarakani serikali ya Rais François Bozizé.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro, mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano ya kikaumu yaliyopelekea kuondolewa madarakani serikali ya Rais François Bozizé.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.