ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 29, 2024

MIRADI YA TRILIONI 8.5 KUTEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU MKOA WA PWANI.

 

VICTOR MASANGU,CHALINZE


Mbio za Mwenge wa Uhuru umewasili leo rasmi mkoani Pwani ukitokea Mkoani Morogoro ambapo umekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo utembelea na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo.

Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge alisema kwamba katika mbio hizo mwenge huo utatembelea jumla ya miradi ipatayo 126.


Kunenge alibainisha kwamba mbio za Mwenge huo wa uhuru kwa mwaka huu  utakimbizwa katika Halmashauri tisa zilizopo katika Wilaya saba  ambapo jumla ya kilometa 1,225.3 zitakimbizwa katika maeneo mbali mbali.

Kunenge alifafanua kwamba kati ya miradi hiyo miradi 18 itawekewa mawe ya msingi,miradi 22 itazinduliwa na miradi ipatayo 86 itakaguliwa.

Aidha Kunenge alisema kuwa miradi hiyo itagharimu  kiasi cha shilingi Trilioni 8.536  ambapo serikali kuu imechangia bilioni 13.6,Halmashauri za wilaya shilingi bilioni 2.3 nguvu za wananchi na wawekezaji trilioni 8.5 na wadau wa maendeleo bilioni 14.6.

Pia alimshukuru Rais wa awamu ya sita kwa kuweka mazingira bora kwa ustawi na ufanisi zaidi katika sekta binafsi nchini.


Pia Kunenge katika hatua nyingine alisema kwamba katika kupambana na janga la ukimwi wameendelea kupambana kwa kutoa elimu ya upimaji wa wenza.

Kadhalika aliongeza katika kupambana na dawa za kulevya wameendelea kuimarisha mapambano kwa kubadilisha fikra,hisia na tabia.

Awali kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Mnzava alizitaka halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaandaa nyaraka zote za miradi ya maendeleo.8

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.