NA ALBERT GSENGO/MWANZA
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba ametoa siku tatu kuanzia Mei 2 hadi Jumapili Mei 5, mwaka huu kwa wafanyabiashara, wenye maegesho mahususi, wamiliki wa vibanda vya maduka kwenye masoko, makampuni ya kuzoa taka na wananchi waliojenga bila vibali kulipa ushuru, kodi na ada mbalimbali za halmashauri hiyo bila shuruti. Kibamba ametoa wito huo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini hapa akisisitiza kwamba amefikia hatua hiyo baada ya kufanya juhudi mbalimbali za kufuatilia ukusanyaji wa mapato kwa njia za kistaarabu lakini wafanyabiashara hao wamekuwa wazito kutii sheria kwa hiari. Amesema kodi zote na ushuru zitalipwa kwenye mfumo wa kielektroniki huku akiwataka wafanyabiashara hao kuepuka kulipa mikononi kwani atakayefanya hivyo malipo yake hayatakubalika na hayatatambulika, hivyo, ili kuepuka usumbufu amewataka kufika ofisini kwake kuchukua namba za malipo (control number). Amesema katika jitihada za kuhamasisha ukusanyaji huo wa kodi na ushuru waliwatumia watendaji wa mitaa kuwafikia wafanyabiashara na watu wote ambao wanafanya shughuli mbalimbali ambazo wanastahili kwa mujibu wa sheria kulipa kodi na ada mbalimbali kwa mujibu wa sheria za halmashauri ya jiji la Mwanza ili kuiwezesha kutoa huduma kwa wnaanchi kwa mujibu wa sheria. #samiasuluhuhassan #jembefm #mwanzaTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.