WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo amesema mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha mkaa mbadala katika eneo la Visegese Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani kitakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuleta mapinduzi ya kupunguza changamoto ya uharibifu wa mazingira ambao ulikuwa unafanyika.
Jafoo alibainisha kwamba mkaa utakaozalishwa katika kiwanda hicho utasaidia wananchi kuachana na kutumia kuni na mkaa unaotokana na kukatwa kwa miti ovyo na kupelekea uharibu wa misitu na kupoteza uoto wa asili uliopo.
Dk.Jafo ameyasema hayo wakati mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa ulipotembelea kiwanda hicho kukagua ujenzi na na kupanda miti katika eneo hilo ambapo alisema mradi huo ni muhimu kwani utakwenda kuokoa hekta zaidi ya 4,622,000 zinazopotea kutokana na vitendo vya kukata miti.
" Mradi huu katika upande mazingira utaleta heshima.kubwa, niwapongeze Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kwa kutekeleza maagizo ya viongozi wakuu katika mapambano ya kutokomeza uharibifu wa mazingira," amesema.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mzava akizungumza katika mradi huo amesema kwakua lengo la mradi ni kuzalisha nishati mbadala Stamico wanatakiwa kuongeza kasi na kusimamia mradi huo utekelezwe kwa viwango na kukamilika kwa muda uliopangwa.
Awali akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Kibaha, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Fatuma Nyangasa amesema Mwenge huo umembizwa km 125.7 na kukagua, kuzindua, na kuweka mawe ya msingi miradi saba yenye thamani ya sh. Biln 3.4.
Pia Mwenge huo umeweka jiwe la Msingi katika mradi wa daraja Makurunge, umekagua maabara ya Ufundi umeme, ushonaji na mapishi pamoja na kuzindua klabu ya wapinga Rushwa.
Miradi mingine ni jengo la mama na mtoto, ambao ulizinduliwa, mradi wa darasa lenye watoto wenye mahitaji maalumu shule ya Msingi Sanze, mradi wa vijana uzalishaji wa Kiwanda
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.