ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 14, 2015

SIMU YASABABISHA AJALI.

 WATU arobaini wamejeruhiwa katika ajali mbaya ya basi la abiria lililoacha njia na kupinduka eneo la kijiji cha Bulalu, kata ya Nyanguge wilayani Magu mkoani Mwanza.

Taarifa za awali zilizotolewa na Diwani wa kata ya Nyanguge wilayani Magu, Hillali Elisha, zilieleza kuwa basi hilo lenye namba za usajili T891DAK liliacha njia na kupinduka likitokea Sirari mkoani Mara likielekea jijini Mwanza.
 "Chanzo cha ajali kimedaiwa kuwa ni mwendo kasi lakini baadhi ya abiria walidai dereva wa gari hilo alikuwa akiongea na simu ya mkononi na mbele kulikuwa na gari dogo la abiria (daladala) ambapo lilipunguza mwendo ambao dereva wa basi hakuustukia kwa kukosa umakini hivyo kwa kasi aliyokuwa nayo ilimlazimu kulikwepa" alisema.

Elisha alisema baada ya kulikwepa daladala hilo, gari hilo lilimshinda na hivyo kuacha njia kisha kupinduka mara mbili na kusababisha majeruhi 40 ambao baadhi wamevunjika miguu, mikono na kuumia sehemu mbalimbali milini, hakuna aliyepoteza maisha. 
Baadhi ya abiria waliopata majereha kwenye ajali hiyo wakiwasiliana na ndugu zao kwa simu.
Wananchi wakiangalia kama kuna abiria wenye kuhitaji msaada waliosalia.
Hali halisi.
Eneo la tukio.
Diwani Elisha amewataka madereva kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani kujiepusha na ajali zinazoepukika ikiwa ni pamoja na kudhibiti mwendo kasi wa vyombo vyao vya usafiri.

Pia amewapongeza wananchi wa eneo la kitongoji cha Bulalu katani Nyanguge kwa kufika eneo la tukio kwa wakati na kutoa msaada kwa abiria huku wakiweka ulinzi wa mizigo ya abiria jambo ambalo limedhihirisha uzalendo mkubwa walionao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.