ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 14, 2024

RC PWANI AMUAPISHA RASMI PETRO MAGOTI KUWA MKUU MPYA WA WILAYA YA KISARAWE

 

NA VICTOR MASANGU,PWANI 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge leo amemuapisha rasmi Petro Magoti kuwa mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe na kumuagiza kwamba anaweka kipaumbele kikubwa katika suala zima la ulinzi na usalama katika maeneo mbali mbali.

 Katika halfa hiyo ya uapisho  imehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali viongozi wa chama,wakurugenzi,wakuuwa Wilaya,wakuu wa idara  pamoja na wageni wengine kutoka sehemu mbali mbali.

Mara baada ya kuapishwa rasmi Mkuu huyo mpya wa Wilaya Petro Magoti alitoa shukrani kwa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kumuamini na kumchagua katika nafasi hiyo.

Mkuu huyo aliahidi kushirikiana bega kwa bega na viongozi wengine wa Wilaya ya Kisarawe pamoja na Mkoa mzima wa Pwani kwa lengo la kuweza kuleta maendeleo kwa wananchi.


"Nashukuru kwa dhati kwa Rais kuweza kunichagua katika nafasi hii na mm nitakuwa mstari wa mbele katika kusaidia na viongozi wenzangu katika kuwatumikia wananchi wa Wilaya ya Kisarawe ",alisema Magoti.

Aidha Magoti alisema kuwa ataonyesha taswira nzuri katika suala zima la uwajibikaji katika uongozi wake na kwamba atayatekeleza yale yote ambayo ameagizwa na Rais  kuyatekeleza  katika sekta mbali mbali.

"Nchi hii ya Tanzania ina watu wengi sana ambao ni wasomi na wengine wana uwezo mkubwa lakini mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kumpendeza na kuamua kunichagua katika nafasi hii na mm namwomba Mungu anijalie niwe mtiifu katika kazi hii,"alifafanua  Magoti.

Kadhalika Mkuu huyo alimwakikishia Mkuu wa Mkoa wa Pwani kumpa ushirikiano wa kutosha yeye pamoja na wasaidizi wake wote.

Magoti aliongeza kuwa katika kutekeleza majukumu yake atahakikisha anafanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi ya kuwa na mshikamano pamoja na utiifu.

Aliwaomba viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wa ngazi zote pamoja na wananchi kufanya kazi kama timu ya pamoja ili kuweza kumsaidia Rais katika mambo mbali mbali.

"Mimi nimefanya kazi Ikulu na Rais wetu kwa kweli anachapa kazi kweli usiku na mchana maana halali kwa hivyo na sisi viongozi tunapaswa kuiga mfano wake katika kutimiza wajibu wetu,"alisema Magoti.

 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kumuapisha Mkuu huyo wa Wilaya alimtaka kusikiliza kero na changamoto mbali mbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Kunenge alisema kwamba katika Wilaya ya Kisarawe kunatakiwa kuangalia vipaumbele ikiwemo suala la kusimamia hali ya ulinzi na usalama kwa wananchi wake.

Pia alimuimiza kutumia muda wake katika kusimamia mambo mbali mbali ya msingi ikiwemo suala kutekeleza katiba ya nchi pamoja na kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo.

Pia Kunenge hakusita kukumbishia suala la ukusanyaji wa mapato ikiwa sambamba na kutangaza vivutio vya utalii vilivyomo katima Wilaya husika na kuweka mikakati ya kuwa na kilimo chenye tija.

 Rais wa awamu ya sita  Dkt Samia Suluhu Hassan hivi karibuni alimteuwa Petro Magoti kuwa mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe ambapo leo amepata fursa ya kuapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.