ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 14, 2024

JUMAPILI HII MWANZA PATACHIMBIKA RC MTANDA USO KWA USO DHIDI YA DC NASSARI

 NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA

Ilianza kama utani lakini hivi lakini sasa inakwenda kuwa nayo historia inakwenda kuandikwa, kwa mara ya kwanza wakazi wa jiji la Miamba (Rock City) Mwanza wanakwenda kushuhudia mtanange wa kukata na shoka baina ya timu ya Veterani ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda dhidi ya timu ya Veterani ya Mkuu wa Wilaya ya Magu Joshua Nassari. Kwa mujibu wa wasemaji ambao pia ni wachezaji wa timu zote mbili wanasema ni uhakika kwamba viongozi hao wawili nao watashuka dimbani kuwa sehemu ya 'First Eleven' ya wachezaji ishirini na mbili wa pande mbili zinazoshuka kupepetana Jumapili ya wiki hii yaani tarehe 16 Juni 2024 katika dimba la Nyamagana jijini hapa, ambapo tayari mashabiki toka ofisi za Serikali toka wilaya za karibu wamepanga kuhudhuria mtanange huo wenye 'KAULI MBIU SHIRIKI MICHEZO ILI KAZI IENDELEE' #mwanza #magu #samiasuluhuhassan

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.