ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 25, 2014

MEYA WA JIJI LA MWANZA NI MMOJA KATI YA WATIMUA VUMBI KESHO ROCK CITY MARATHON CCM KIRUMBA


MWANZA.
Baada ya kuutangaza mwezi mzima wa usajili kwa washiriki, hatimaye leo dirisha la kusajiri washiriki wa mbio za Rock City Marathon kupitia mitandao na analojia, limefungwa rasmi ikiwa ni masaa machache kwa mashindano hayo kuanza kutimua vumbi.

Mathew Kasonta ambaye ni mratibu wa Rock City Marathon, amewataka washiriki waliojisajili kushiriki mbio hizo kufika mapema kesho Jumapili (26/10/2014) asubuhi katika uwanja wa CCM Kirumba ili kuweza kushiriki kikamilifu na kwa tija, kuufufua mchezo huo, kuvibaini vipaji ikiwa ni pamoja na kunyanyua hamasha ya wapenzi na mashabiki wa mchezo huo ambao katika zama za baadaye ndiyo walezi. BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza akionesha fomu yake ya usajili kushiriki mbio za Rock City Marathon.
Zaidi ya shilingi milioni 9 zimetengwa kama sehemu ya zawadi kwa mbio za Rock City Marathon ambapo mbali na washiriki kutoka ndani ya nchi washiriki wengine ni kutoka nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na sehemu mbalimbali toka kwa mabara tofauti duniani ambapo vilevile Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula atakuwa ni mmoja wa washiriki wa mbio hizo.

Mabula alikuwa mtu wa kwanza kuchukuwa fomu ya ushiriki na kuijaza ikiwa ni kipindi cha takribani mwezi mmoja sasa. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.