ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 28, 2018

HALI NI SHWARI SASA KATIKA ENEO AMBALO ABIRIA WALIKUWA WAKIVAMIA MAJIRA YA ASUBUHI NA KUFANYIWA VITENDO VYA UNYAMANA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Baada ya kupitia kipindi kigumu cha hali ya sintofahamu katika usalama kwa takribani miezi mitatu toka mwishoni mwa mwaka jana 2017 mwezi wa 12 na mwanzoni mwa mwaka 2018 kwa mwezi wa kwanza na wa pili, hatimaye sasa hali ya amani imerejea katika eneo la Nyegezi lililopo ndani ya wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Jeshi la Wananchi mkoani hapa mkono kwa mkono kwa kushirikiana na wananchi wamefanikisha kujenga kituo cha polisi kwa ajili ya ulinzi na kutoa usaidizi.

Hili ni eneo ambalo wananchi waliokuwa wakiamka alfajiri kwenda kwenye vituo vya mabasi walikuwa wakivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa nondo, huku kukiripotiwa vifo na baadhi yao kupata vilema vya maisha.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.