ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 30, 2018

SASA NI KOMBE LA DUNIA BILA MESSI WALA RONALDO.


.....Ulimwengu hii leo umeshuhudia tukio kubwa la simulizi dunia, kwa mastaa wa Modern football Messi na Ronaldo kuiaga #Urusi .
FT #France 4-3 #Argentina
FT #Uruguay 2-1 #Portugal .
.
Wakali wa mambo wanasema huenda ikawa mwisho wa utawala wao Jeh nawe unamaoni gani? #SportsRipoti @elikanamathias & @danyajr_219

UFARANSA V ARGENTINA
Ufaransa imetua robo fainali ya Kombe la Dunia mara ya pili mfululizo na kubadili historia kufuatia ushindi kwenye mchuano wa kuvutia uwanjani Kazan dhidi ya Argentina.

Argentina, iliyokuwa na baadhi ya wachezaji bora duniani, Lionel Messi na Diego Maradona ugani Kazan, mmoja akicheza mwingine akiwashangilia, wameliaga Kombe la Dunia Urusi 2018.

Mabao ya haraka ya Kijana chipukizi Kylian Mbappe kipindi cha pili yameipa Les Bleus tiketi ya robo fainali Urusi 2018.

Ufaransa inamsubiri mshindi kati ya Uruguay na Ureno watakaokwatuana baadaye.

Ufaransa iliingia mechini vyema kwa kuchukua uongozi baada ya mlinzi Marcos Rojo kumuangusha Mbappe.

Griezmann alitandika Penalti hiyo na kujaa kimiani (dakika ya 13).

Hata hivyo, dakika chache kabla ya kipindi cha pili, Angel Di Maria aliisawazishia Argentina kwa shuti la ajabu kutoka yadi 30 na kumaliza kipindi cha pili kwa sare 1-1.

Punde tu pande hizo ziliporejea kutoka mapumziko, beki Gabriel Mercado aliinyakulia Argentina uongozi (Dakika ya 48) baada ya kuulekeza mkwaju wa Messi langoni.

Sherehe za Albiceleste zilikatizwa baadaye kwani uzembe wa ngome yake ilimruhusu beki Benjamin Pavard, aliyekuwa akishiriki mechi yake ya tisa kwa timu ya taifa, kuisawazishia Ufaransa. Pavard alifunga Dakika ya 58.

Ngoma ilionekana kumalizika sare kabla ya nyota wa PSG Mbappe kuidunisha Argentina kwa mabao ya haraka dakika za (64) na (68) na kuwainua mashabiki wa Ufaransa kutoka viti vyao.

Lionel Messi alijaribu kupunguza madeni ya Argentina kufuatia mabao hayo lakini mbio zake kwenye sanduku ziliandamwa na shuti lake dhaifu hadi kwa viganja vya mdakaji wa Ufaransa Lloris.

Argentina bao la tatu

Hata hivyo dakika chache baadaye Messi hakuchelea kumlisha Aguero naye nguvu huyo mpya, Kun Aguero alipiga kichwa safi dakika ya 92 na kukaribia kufufua matumaini ya Argentina.

Muda haukuwa na huruma kwa Argentina na kipute kilikamilika ushindi ukienda kwa Ufaransa.


Mjadala wa ni nani bora kati ya Messi na Ronaldo benchi kwa sasa.

Argentina na Ureno wameliaga Kombe la Dunia.

Ukurasa mpya umefunguliwa kwa mashabiki wa soka duniani kuhusu ubora wa wachezaji maarufu wa soka.
Ingawa kila mwamba ngoma, ngozi huivutia kwake, ukweli ni kuwa, wachezaji wapya wametumia vyema jukwaa lililopatikana Kombe la Dunia Urusi 2018.
Baada ya kutawala vinywa vya wengi ndani ya zaidi ya kipindi cha miaka 10, kuondoka kwa Argentina na Ureno Urusi hatua za mchujo, imewanyima Messi na Ronaldo muda zaidi wa kujadiliwa.
Kurunzi za soka sasa zimeelekezwa kwa Neymar wa Brazil, Paul Pogba, Kylian Mbappe na Antoine Griezmann wa Ufaransa, Edison Cavani na Luis Suarez wa Uruguay, Harry Kane wa Uingereza na Romelu Lukaku wa Ubelgiji.
Orodha ni ndefu, lakini yote yataamuliwa kulingana na mchango wa wachezaji hawa kwa ufanisi wa timu zao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.