Kangi Lugola. |
Rais John Magufuli amemteua Mbunge wa Mwibara na aliyekuwa Naibu waziri wa Muungano na Mazingira, Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akichukua nafasi ya Mwigulu Nchemba.
Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo mchana huu kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi John Willium Kijazi.
Mwigulu Nchemba. |
Taarifa hiyo imesema kwamba nafasi ya Kangi Lugola inaenda kuchukuliwa na Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Ramadhan Sima.
Aidha Rais amefanya uteuzi wa Naibu Waziri katika Wizara ya kilimo kutokana na umuhumu wa Wizara hiyo ambapo, Mbunge wa Morogoro Kusini Omary Mgumba ameteuliwa kushika nafasi hiyo.
Pamoja na hayo, katika mabadiliko hayo madogo, Rais Mgufuli amefanya Uhamisho Waziri Prof. Makame Mbarawa kutokea Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anaenda kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, huku aliyekuwa kwenye Wizara hiyo, Mhandisi Isack Kamwelwe anaenda kuwa Waziri wa Uchukuzi.
Hata hivyo Balozi Kijazi amesema tarehe ya kuapishwa kwa viongozi hao itatajwa hapo baadaye
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.