NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Kakika juhudi za kumuunga mkono RAIS MAGUFULI kuelekea
tanzania ya viwanda, Serikali imeombwa kuwajengea uwezo wajasiriamali na kuondoa
bidhaa feki kwenye soko pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria
wafanyabiashara wanaonakili nembo na uzalishaji wa bidhaa zao kinyume cha sheria.
Kilio hicho kimetolewa na
wafanyabishara wa jijini Mwanza wanaozalisha vinywaji aina ya Wine zinazotokana
na matunda pamoja na mtama.
Aidha meneja wa (TFDA) kanda ya ziwa MOSES MBAMBE,amewataka
wananchi kutoa ushirikiano pale wanapoona
bidhaa ambayo wanaitilia sahaka nakuwataka wajasilia mali kurasimisha bidhaazao
ili zitambulike na (TFDA) pia mbambe amesema kwa sasa wanaendelea kutoa elimu
kwa wajasiliamali wa kanda ya ziwa.
Mkurugenzi wa kiwanda cha Mwanza quality wine Leonald Lema
amesema kuwa mamlaka zinazohusika
zinapashwa kuingilia kati kwani bidhaa feki zinawaathiri wao pia maptao kodi ya
serikali.
Aidha LEMA amebainisha kuwa kiwanda chake hakina tatizo la
vifungashio tatizo ambalo limekuwa likipigiwa kelele kuwa bidhaa nyingi hapa
nchini zinakosa ubora katika ushindani kwenye soko ukilinganisha na bidhaa toka
nje.
Naye Mkurugenzi wa FARU WINES Japhet Daniel amesema kuwa
serikali kwa kutumia mihili yake inaweza kuwatambua wajasiriamali wasio
sajiliwa kutumia vifungashio vya bidhaa za FARU BANANA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.