Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo amepokea *shehena ya Vifaa vya matibabu* vyenye thamani ya shilingi *milioni 100* kutoka serikali ya *Korea Kusini* kupitia shirika la *KOICA*.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na *Digital X-ray 3, Ultrasound 1, Kabati la usalama wa viumbe* (safety cabinet) 1, *Mashine 3 za kupima mkojo, mashine ya kuwapa joto watoto njiti* (baby warmer) pamoja na *mashine ya utakitshaji.*
Baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka kwa *Balozi wa Korea kusini Bwana Geum Young Song RC Makonda* amekabidhi vifaa hivyo kwenye *vituo vya Afya vya Sinza, Mnazi Mmoja na Mbagala* ambako kuna uhaba wa vifaa. Kabla ya kupokea vifaa hivyo *RC Makonda* alifanya *mazungumzo* na *Balozi* huyo wa Korea kusini na kuwasilisha *ombi la kujengwa kwa Chuo cha kisasa cha mafunzo ya udaktari na uuguzi* ambapo *Balozi Geum Young Song amepokea kwa mikono miwili ombi hilo.*
*RC Makonda* pia amemueleza Balozi ombi la kujengwa kwa *kituo kikubwa cha upimaji wa magonjwa mbalimbali* kwa wananchi kwenye *eneo moja* ambapo pia Balozi *amepokea* ombi hilo na kumsifu *RC Makonda* kwa moyo wake wa kujali wananchi.
Kwa upande wake *Balozi* wa Korea Kusini nchini Tanzania *Bwana Geum Young Song* amesema wametoa vifaa hivyo *kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Mkoa wa Dar es salaam katika uboreshaji wa sekta ya Afya* na wataendelea kusaidiana na serikali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.