ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 30, 2018

MAMBO MUHIMU YANAYOPATIKANA KATIKA RIPOTI YA UTAFITI WA UHISANI NCHINI ILIYOANDALIWA NA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Mchambuzi na mwandishi wa ripoti ya utafiti wa Uhisania Tanzania Bw. Tom Were akiichambua ripoti hiyo mapema jana jiji Dar es salaam.

Watanzania wametakiwa kuwa na moyo wa kutoa kwa kusaidiana wenyewe ndani ya jamii na hata katika kuendeleza huduma mbalimbali za kijamii ili kuweza kusaidia taifa kusonga mbele.


Hayo yamesemwa mapema jana jijini Dar es salaam na Mwanachama wa Bodi ya wakurugenzi ya Foundation for Civil Society Bi. Nesia Mahenge wakati wa uzinduzi wa riporti ya utafiti maalum kuhusu uhisani na utamaduni wa kujitolea ndani ya Tanzania.

Ripoti hiyo iliyohusisha utafiti uliofanywa kati ya mwezi februari hadi mwezi aprili na kuhusisha mashirika ya Foundation for Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na Jukwaa la Uhisani Tanzania (Tanzania Philanthropy Forum) kwa lengo la kupata taarifa muhimu kuhusu hali ya uhisani au hali ya kujitolea kwa jamii nchini Tanzania.
Mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya Foundation for Civil Society Nesia Mahenge akielezea kwa undani mambo yanayopatikana katika ripoti hiyo ya Utafiti wa Uhisani nchini Tanzania.

Mwanachama wa bodi huyo alisisitiza umuhimu wa mtu mmoja mmoja  pamoja na taasisi mbalimbali binafsi hususani zinazofanya kazi za kijamii kuendelea kujitolea katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kuacha tabia ya kuisubiri serikali kufanya kila kitu.

Aliendelea kusisitiza kuwa ni vema kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo ikiwa ni moja wapo ya njia nzuri ya kuisaidia serikali katika kuinua miradi kadhaa ikiwemo Elimu, Afya, Ujenzi na sio kwa kuwezesha kifedha tu lakini hata katika kusaidia kuleta wahisani watakao fanikisha zoezi hilo pia ni hatua kubwa.

“Lakini pia katika hali ya kujitolea kwa Tanzania uelekeo wake sio mbaya sana kwani watanzania wanaonyesha kuwa wana moyo wa kutoa kwa kusaidiana, lakini pia hata katika juhudi za kujiletea maendeleo kwa kusaidia huduma mbalimbali za kijamii hali inaonyesha bado tupo vizuri” alisema Nesia
Wachambuzi wakiichambua Ripoti ya Utafiti wa Uhisani Tanzania 

Aliongezea kwamba tatizo moja linalojitokeza katika nchi yetu ni kwamba kunakosekana takwimu/taarifa sahihi za watu wanaojitolea lakini zingekuwepo ingesaidia kujua kiwango husika cha watu wanaojitolea katika miradi ndani ya jamii yao na hii inatokana na sharia na mifumo iliyowekwa ndani ya nchi yetu.

Na mwisho alipenda kuwashauri wadau kutumia matokeo ya utafiti huu kama sehemu ya kubadilishana uzoefu katika tasnia nzima ya uhisani na kujitolea katika jamii na kuhamasisha umuhimu wa uhisani miongoni mwa jamii ya watoaji pia kuweka muongozo wa kuendeleza uhisani Tanzania.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini uchambuzi wa Ripoti ya uhisani Tanzania iliyozindiliwa na Foundation for Civil Society mapama jana jijini Dar es salaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.