ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 28, 2018

MAPEMA LEO ASUBUHI MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA ZIMBABWE


Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa amewasili leo Alhamisi Juni 28, 2018 saa 5:30 asubuhi katika uwanja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli.
Baada ya kuwasili amepigiwa mizinga 21, kukagua gwaride la heshima.
Mbali na Rais Magufuli, viongozi wengine waliofika kumpokea rais huyo wa Zimbabwe ni Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi;  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba;  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Baada ya mapokezi ya uwanjani, marais  hao wameelekea Ikulu kwa mazungumzo zaidi.
JEH ZIARA YA RAIS WA ZIMBABWE INA MANUFAA GANI KWA TANZANIA?
Katika taarifa kutoka ikulu Tanzania, Rais Magufuli amesema wamekubaliana tume ya pamoja ya ushirikiano, iliyokutana mwisho mnamo 1998, ikutane mara baada ya uchaguzi mkuu wa Zimbabwe mwezi ujao ili kujadili vikwazo na kutafuta majawabu ya kukuza biashara na uwekezaji baina ya Mataifa haya mawili.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Tanzania, Said Msonga anaamini huenda Rais Mnangagwa anatumia ziara hii kama mbinu ya kutaka kuibua hisia za wanamchi na kutaka kuonekana mzalendo na kumtengenezea mazingira ya kushinda uchaguzi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.