GSENGOtV
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana la KIVULINI Yasini Ally amesema haiingii akilini kwa mkulima aliyeuza mazao yake na kupata mamilioni ya fedha ashindwe kununua hata godoro, zaidi ya kukimbilia kununua magodoro yaliyotengenezwa kienyeji kwa kutumia mifuko ya magunia ya saflet iliyoshindiliwa makapi ya majani ya mpunga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi mkoani Mwanza, Eliurd Mwiteleke amesema kuwa Halmashauri yake inatarajia kuanza kampeni maalum inayolenga kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto, wanawake na wazee ambayo itakayodumu kwa kipindi cha miezi miwili.
Kauli hiyo inatoka ndani ya kongamano la mafunzo ya jinsi ya kubaini na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii lililoandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Misungwi kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI shughuli ikifanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Misungwi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kitaifa wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia.
Wadau mbalimbali hapa wanapata fursa ya kuchangia.
Sehemu ya kusanyiko mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Idara, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Madiwani, Mahakama, Polisi pamoja na Sungusungu.
Kwa umakini elimu inapenya kwa wadau.
Kusanyiko na tafakari.
Kwa umakini elimu inapenya kwa wadau.
Kwa umakini elimu inapenya kwa wadau.
Wadau wa mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi mkoani Mwanza, Eliurd Mwiteleke, wakati akiwasilisha mada kwenye darasa.
Wadau waliketi kulingana na vitengo vyao ni wasaa wa kuainisha changamoto, kujenga hoja na kuweka mikakati.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.