MKUU wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ameyashukia baaadhi ya makampuni binafsi ya ulinzi mkoani Mwanza kutokana na tabia yao ya kutowasilisha michango ya waajili wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kuitaka mifuko hiyo kuyachukulia hatua kali ili iwe fundisho kwao.
PPF PLAZA MWANZA, MOJA YA VITEGAUCHUMI KWA MFUKO HUO.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza amesema kuwa kwa siku amekuwa akipokea wastani wa malalamiko 10 toka kwa walinzi wa makampuni binafsi wakilalamikia kufukuzwa kazi na waajili wao kushindwa kuwalipa mafao yao ambayo walikatwa kwa mujibu wa sheria huku waajili nao wakitakiwa kuchangia katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
MENEJA WA KANDA BW. BANDAWE.
Kwa upande wake meneja wa PPF Kanda ya ziwa Meshack Bandawe alisema kuwa PPF imekuwa ikiendesha semina hiyo kwa waajili na wadau wake mbalimbali mara moja kila mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu muhimu juu ya mfuko huo.
WASHIRIKI KUTOKA MKOA WA SHINYANGA.
Kuhusu PPF Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza almeupongeza mfuko huo kwa jinsi unavyofanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa na kutoa changamoto kwa mfuko huo kuendelea kuwekeza miradi yenye gharama nafuu kama nyumba ambazo zilijengwa mkoani Mwanza ambazo ziliwavutia wananchi wengi na kununuliwa haraka.
Waajili wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa nafasi kwa wafanyakazi wao kujiunga katika vyama vya wafanyakazi kwa kuwa ni wajibu wao kisheria.
Akijibu swali kwanini waajiri wengi kukwepa kuwaandikisha wafanyakazi wao katika mfuko wa mafao, BEATRICE MINJA HRM MAJOUR DRILLING TANZANIA amesema kuwa tatizo hilo huwa analisikia kutoka baadhi ya makampuni lakini kwa upande wa kampuni yake kabla ya kumwajiri mfanyakazi humpa ufafanuzi juu ya haki zake za msingi, kiasi anachotozwa na nini mafao yake katika ugonjwa, malezi ya mtoto na kadhalika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.