Mzee Muhidin Gurumo ni baba mwanzilishi wa bendi ya Nuta Jazz ambayo sasa "Msondo Ngoma Music Band" aka Baba wa Mziki, aka Mambo hadharani.
Anko Muhidini Maalimu Gurumo amekuwa katika medani ya mziki kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1950s rasmi mwaka 1960 na akiwa moja ya wanamziki wanzilishi wa Nuta jazz band 1964, kabla ya kubadili jina na kuitwa JUWATA JAZZ ikiwa chini ya chama cha wafanyakazi.
Anko Gurumo ni mwanamziki mtunzi,mwimbaji mkongwe na mbunifu wa mtindo mbali ya dansi kama vile Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae (alipokuwa Mlimani Park) na Ndekule (alipohamia kwa muda Orchestra Safari Sound wana OSS) n.k yeye akiwa ndie anayetoa majina haya.
Mzee Gurumo ni Baba wa mziki wa dansi nchini na pamoja kuwa amewahi kupigia bendi nyingi lakini "Msondo Ngoma Music Band" ndiyo ngome yake.
Ras Makunja na Globu ya Jamii inamwomba Mwenyezi Mungu ampe afueni Kamanda wetu Mzee Gurumo. Na pia wadau wa muziki tujitokeze kumsaidia.
HABARI KWA HISANI YA MICHUZI:
Tupe maoni yako
Sasa breking news ya nini hapa, utafikiri mtu hayupo,kwani kuumwa si kitu cha kawaida mtu anatibiwa na kurudi nyumbani.msipende kushtua watu.
ReplyDelete