ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 27, 2010

AJALI YA PIKIPIKI USIOMBEE!!!

AKILIA KWA MAUMIVU MAKALI SIKU YA JANA NILIMKUTA JAMAA HUYU KITUO CHA KATI CHA POLISI MWANZA AKICHUKUWA SICK SHEET MARA BAADA YA KUUMIA KATIKA AJALI YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA.
Kasi ya ununuzi wa pikipiki kwa ajili ya kuzikodisha na matumizi binafsi, inazidi kuongezeka huku kukiwa hakuna tahadhari ya kutosha kuhakikisha wanaoendesha vyombo hivyo vya moto, wamepata mafunzo stahiki.
AMEVUNJIKA KABISA MGUU WA KULIA NA KUKIFANYA KIPANDE CHA CHINI KIKINING'INIA KUMAANISHA KUPOTEZA USHIRIKIANO.
TAARIFA kwamba katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, zaidi ya watu 181 wamefariki kwa ajali ya pikipiki maarufu kwa jina la Bodaboda, ni taarifa za mshtuko na si za kubeza. Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abass Kandoro nakumbuka alipata kuzungumza katika wiki ya nenda kwa usalama iliyomalizika mwezi wa nane 2010 alisema vifo vya watu hao vimesababishwa na ajali za pikipiki zaidi ya 1,414 zilizoripotiwa.

Zaidi ya asilimia 80 ya madereva wa daladala, pikipiki, magari binafsi na mabasi yaendayo mikoani, hawana sifa za udereva na mamlaka husika zimefumbia macho tatizo hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.