Katika kumkwamua mfanyakazina adha aipatayo ya kukabiliana na hali ngumu ya maisha kutokana na kutokuwa na kipato cha kutosha kuweza kujikimu na maisha mara baada ya kuondoka kwenye ajira, Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF kanda ya ziwa umeamua kukutana na waajiri kwania ya kuwapatia semina ili watambue umuhimu na wajibu wao kisheria wa kuandikisha wafanyakazi wao. Meneja wa PPF kanda ya ziwa bw.Meshark Bandawe amesema kuwa moja ya changamoto kubwa inayoikabili sekta nzima ya hifadhi ya mfuko huo wa jamii ni waajiri wengi kutofikisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati. Sambamba na kutoa darasa kwa waajiri hao bw. Bandawe amesema kuwa semina hiyo itatoa maelezo kwa kina juu ya huduma mpya zitolewazo na mfuko huo, kuvielezea vitega uchumi vilivyopo sambamba na kupokea ushauri na mapendekezo juu ya utoaji wa huduma za PPF kanda ya ziwa kwa nia ya kuziboresha hivyo kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
SEMINA HIYO YA KANDA YA ZIWA KATI YA PPF NA WAAJIRI INATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMATATU YA TAREHE 29NOVEMBER 2010 LAKAIRO HOTEL JIJINI MWANZA.
MSD YATUNUKIWA TUZO YA UMAHIRI WA UTOAJI HUDUMA
-
Bohari ya Dawa (MSD), imetunukiwa tuzo ya umahiri wa utoaji huduma kwenye
sekta ya Famasi nchini (Award of Service Excellence in Pharmaceutical
Sector) k...
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.