ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Ukerewe ni kisiwa kikubwa kuliko vyote miongoni mwa visiwa vilivyomo ndani ya Ziwa Victoria na pia ni kisiwa kikubwa kuliko vyote miongoni mwa visiwa vyote vilivyomo kwenye maziwa katika bara lote la Afrika.
Kisiwa hiki kina ukubwa wa kilometa za mraba zipatazo 530. Kisiwa hiki kinaunda wilaya ya Ukerewe ambayo ni moja wapo kati ya wilaya saba za mkoa wa Mwanza. na kipo kilomita 45 kaskazini mwa jiji la Mwanza kikimiliki visiwa vidogo zaidi ya 30.
Baada ya kumaliza siku tatu za maonesho ya makampuni mbalimbali ya kimataifa yenye kuunda ndege zisizokuwa na rubani, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ambaye ni mmoja ya wadau wakubwa wa mradi huo anasema haya......
"Kijiografia Mwanza ni kubwa na sifa hiyo inanogeshwa na uwepo wa visiwa zaidi ya 30 vinavyomilikiwa na mkoa wetu, pamoja na juhudi kubwa za Serikali katika kuboresha huduma za mawasiliano ya miundombinu ya barabara na safari ya njia ya maji hivyo kurahisisha huduma nyingine kama biashara na uchumi lakini bado miundo mbinu hiyo haijawa suluhu linapokuja suala la afya ambalo linahitaji dharula ya haraka"
"Baada ya kuumiza kichwa kwa kufikiri tukihangaika kusaka suluhisho la kudumu litakalo harakisha huduma kwenye vituo ili kuepusha vifo vya akinamama na watoto wanaokosa huduma za haraka, tofauti na helkopta na ndege kubwa ambazo zinahitaji gharama kubwa, ndipo likaja wazo hili la kutumia ndege zisizokuwa na rubani yaani drone" ZAIDI BOFYA PLAYA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.