ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 3, 2018

DIAMOND PLATNUMZ, RAYVANY WAFANYA VIDEO YAO YA KWANZA JIJINI MWANZA.

Mapema jana mwanamuziki mahiri barani Afrika anayetikisa dunia Diamond Platnumz ametua jijini Mwanza na kufanya video yake ya kwanza jijini hapa, akitumia lokesheni mbalimbali zinazo litangaza jiji hili la miamba.
Akiwa ameambatana na mkali mwingine kutoka WCB, aitwaye Rayvany, ambaye wameshirikiana katika ngoma mpya wanayoifanyia kichupa, siku za karibuni wanataraji kuwastua wengi kwa pishi waliloliandaa ambalo kwa mujibu wa vyanzo vyetu limelenga burudani zaidi na kuwarusha mashabiki.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akiwakaribisha Diamond Platnumz na Rayvany katika ofisi zake kwaajili ya mazungumzo mafupi.
Kwa kutambua na kuthamini mchango wa sanaa, hasa kazi nzuri ambayo inafanywa na wakali hao, makaribisho yamekuwa ya kipekee sana.
Utambulisho kwa wadau muhimu.












Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.