ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, November 4, 2018

SERIKALI YATOA KAULI KUHUSU UJENZI WA MFUMO WA RELI YA KISASA.




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mfumo wa reli ya kisasa (SGR) inayojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi reli ambayo inajengwa lengo lake likiwa ni kuboresha uhusiano wa biashara baina ya mikoa itakayoguswa na reli hiyo.

 Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 ambacho kilitakiwa kukamilika Julai 2019, wataalamu watakamilisha Aprili 2019.

“Nimeridhishwa na viwango na maendeleo ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii. Serikali inataka kuona malengo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka kuona SGR inakamilika na kuanza kutumika nchini yanatimia.” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Kuhusu suala la ajira, Waziri Mkuu amesema asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika mradi huo ni watanzania huku amewataka wawe mabalozi wazuri.

“Watanzania mnaofanya kazi katika mradi huu hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa bidii, uaminifu na muwe mabalozi wazuri ili wengine waweze kupata ajira.” Ameongeza Majaliwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.