Siku Moja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro kukabidhiwa orodha ya Majina ya Vigogo ambao baadhi ni viongozi wa Kanisa la Baptist wanaotuhumiwa kutumia vibaya Fedha Za Chuo Kikuu Cha Mount Meru kiasi Cha Bilioni 3 tayari kazi ya kuwatafuta imeanza na tayari aliekuwa mkuu wa kwanza wa chuo hicho Bwana HARRISON OLAN’G amekamatwa na jeshi Polisi Wilayani Arumeru Kwa ajili ya Mahojiano.
Akizungumzia tukio la kukamwata Kwa mtuhumiwa huyo wa kwanza Muhimu, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro amesema wao walipokea maombi kutoka kwa Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la Baptist Tanzania Mchungaji ARNOLD MANASE kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wote wa Ubadhirifu wa Mali Za chuo Kikuu Cha Kanisa la Baptist Cha Mount Meru University ambao wanatuhumiwa kuhujumu zaidi ya Shilingi Bilioni 3 Za chuo hatua iliyosababisha chuo kushindwa kujiendesha na hatimae kufungiwa na TCU
Mhe Muro amesema wao kama serikali wanatekeleza ombi la Kanisa la kuomba kuingilia kati sakata hilo ili haki itendeke na kusisitiza kuwa tayari ameshatoa maelekezo Kwa jeshi la Polisi kuendelea kuwasaka watuhumiwa wengine na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria ili haki itendeke.
“Kazi inaendelea, tunaomba ushirikiano wa wananchi katika kuwabaini wengine” amesema Mhe Muro.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.