Mabingwa wapya wa ligi kuu soka nchini Kenya (KPL), Gor Mahia wameondoka asubuhi ya leo kuelekea nchini Uingereza kwaajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Everton.
Gor Mahia inatarajia kukipiga na Everton usiku wa Jumanne ya wiki ijayo katika uwanja wa Goodson Park.
Pia inaelezwa kuwa moja ya ratiba ya Gor Mahia nchini humo ni kutazama mchezo wa ligi kuu (EPL) kati ya Everton na Brighton & Hove Albion, mchezo utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii kwenye uwanja huohuo wa Goodson Park.
Mchezo huo ni katika muendelezo wa mashindano ya Sporti Pesa yaliyofanyika mwanzoni mwa mwezi Agosti yakihusisha vilabu kadhaa vya Afrika Mashariki ili kumpata mshindi mmoja atakayekutana na Everton.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.