ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 26, 2022

DC MOYO ATAKA VIONGOZI WA DINI NA KIMILA KUSHIRIKISHWA KAMPENI YA CHANJO YA POLIO

 

Mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wajumbe wa chanjo ya polio Manispaa ya Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa kupitia idara ya afya Inatarajia kutoa chanjo ya Ugonjwa wa polio kwa watoto 25 elfu walio chini ya umri wa miaka mitano (5) ili kuwakinga na hatari ya kuambukizwa virusi vya maradhi hayo

Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Dr. Baraka alisema kuwa Halmashauri hiyo tayari imepokea dozi 27 elfu za kinga ya Polio na kwamba zoezi la chanjo litaanza kutekelezwa kuanzia April 28 hadi mei mosi mwaka huu.

Wakati wa mafunzo kwa kamati ya msingi ya huduma za afya kwa jamii Mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amehimiza viongozi wa dini kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa chanjo hiyo kwa watoto.

Dr. Chaula alisema kuwa lengo la kutoa mafunzo hayo ni kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya umuhimu wa wazazi na jamii kwa ujumla juu ya kuwapatia chanjo ya polio watoto wao.

Alisema kuwa ugonjwa wa polio unataja kuathiri watoto wenye umri wa miaka chini ya kumi na nne lakini kwa mujibu wa wataalam wa afya ugonjwa huo uathiri zaidi watoto walio chini ya umri wa miaka mitano

Dr. Chaula alisema kuwa tayari chanjo zimekuwishapokelewa katika manispaa ya Iringa kilichosalioa ni utekelezwaji wa zoezi lakutoa chanjo kwa wahusika

Mganga mkuu wa Manispaaya Iringa ameyasema haya wakatiwa akimkaribisha mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo katika uzinduzi wa kampeni hiyo yaChanjo.

Kwa upande wake mgeni wa Heshima mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ni lazima kuwashilikisha viongozi wa mitaa ili waone umuhimu wa jambo hilo.

Alisema kuwa kuwashirikisha viongozi wa ngazi ya mtaa hadi kata kutasaidia kufanikisha zoezi hilo la chanjo ya polio kwa watoto wadogo na jamii kulijua swala hilo la polio.

Moyo aliwaomba viongozi wa dini wilaya ya Iringa kulichukua swala la polio kama la kwao kwa kuwaelimisha jamii juu ya chanjo ya polio kuwa ni chanjo salama ambayo inawakinga woto wao.

Aliwaomba wananchi kushiriki katika kampeni ya chanjo ya polio kwa watoto wadogo ambao ndio waathirika wakubwa na chanjo hizo zipo kwa ajili ya kuwakinga watoto wao.

Mkuu huyo wa wilaya alimazia kwa kumuagiza mganga mkuu wa manispaa ya Iringa kuhakikisha anaishirikisha jamii na viongozi wa dini na viongozi wa kimila ili waweze kusaidia kufikisha ujumbe kwa wananchi husika.

 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.