Familia ya mlinzi anayedaiwa kuuawa na mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Pendael Molllel imeliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua za kisheria kwa wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.
Imesema kuwa imepanga kufanya maziko ya ndugu yao Jimmy Mollel (43), Aprili 26, Ngaramtoni wilayani Arumeru, baada ya mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, mjomba wa marehemu, Ernest Julias alisema licha ya kuridhia kumzika ndugu yao wanaliomba jeshi hilo kufanya uchunguzi na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.
“Nilimpigia RCO ameniambia majibu ya postmoterm (uchunguzi) ni kwa ajili ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi na sisi tumeridhika na tunatarajia kumzika nduyu yetu Jumanne ijayo eneo la Ngaramtoni, wilayani Arumeru,” alisema.
Alisema taarifa waliyoipata kutoka kwa daktari ilionyesha kuwa chanzo cha kifo ni maumivu makali yaliyosababishwa na jeraha alilonalo marehemu kwenye kisogo ambapo inaonekana alipigwa au kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
Kamanda Polisi mkoani Arusha, Justine Masejo, amethibitisha kukamatwa kwa Mollel na wenzake watatu Mjini Moshi walikokimbilia kwenda kujificha, wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.