NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Moshi
DAKTARI
bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and
Immunology), Profesa John Shao, ameelezea uzoefu wake juu ya mahangaiko waliyokumbana nayo
wafanyaakzi walioumia wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi inapofikia muda wa
kulipwa fidia.
Akitoa
uzoefu huo mbele ya madaktari wanaoshiriki mafunzo ya siku tano (5) ya tathmini
ya Mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana
na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka Kanda ya Kaskazini mjini Moshi
Februari 21, 2018, Profesa Shao ambaye kwa sasa amestafu kazi, alisema uwepo wa
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), utawezesha wafanyakazi walioumia kazini kwa
mazingira mbalimbali waweze kupata haki zao stahiki.
Ukosefu
wa wataalamu wenye ujuzi wa kufanya tathmini wakati huo, kulipelekea shida
nyingi kwa wafanyakazi waliopata madhara kazini.
Aidha
Profesa Shao ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye taasisi za tiba akiwa
kama Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC Moshi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Tumaini, na pia aliwahi kufanya kazi Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiwa ni
pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Mawenzi na Hospitali ya
Karatu, aliushauri Mfuko katika kutekeleza majukumu yake ni lazima sasa ujikite
katika mambo ambayo aliyaona wakati huo yakiwa na mapungufu.
“Kuwe
na utaratibu katika ngazi ya vituo vya afya vya binafsi na vya serikali ambavyo
vitawapokea wagonjwa kama hawa na kuwapima kutokana na jinsi walivyoumia na
kuwapatia rufaa ya kwenda katika hospitali za wilaya, mkoa au hizi za madaktari
bingwa ili waweze kupata huduma hiyo na vile vile kutathminiwa kwa usahihi.”
Alisema.
Alishauri
kuwa kazi hii ya kufanya tathmini isiachiwe kwa Daktari mmoja au muuguzi mmoja
au afisa mmoja tu bali pawepo na kikundi (team work) ambacho kimepata mafunzo
mazuri kinachoweza kupima na kutoa muelekeo mzima na katika kufanikisha hili
lazima pawepo na mfumo mzuri endelevu wa mafunzo kama haya.
“Uwepo
mfumo wa wataalamu (madaktari) wanaopata mafunzo haya watoke kila kada ili wapatiwe
mafunzo stahiki ya kuwahudumia wagonjwa wanaopata madhara yatokanayo na kazi,
ili wawe na uwezo wa kutoa tathmini iliyo sahihi.
Pia
alishauri kuwepo na mfumo wa kuimarisha uanzishwaji viwanda walau kuwe na Minimum Standard ya viwanda vinavyoanzishwa
vikidhi mazingira salama ya kazi na hatua hiyo iende sambamba na mafunzo kwa
wafanyakazi walioajiriwa wawe na muda wa kupewa elimu ya madhara yanayoweza
kutokea kwenye mazingira yao ya kazi na jinsi gani wanaweza kujiepusha nayo.
Aidha
gwiji huyo wa uchunguzi wa vijidudu na madawa, aliwaasa madaktari hao kutoka
mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara, kufanya kazi kwa uadilifu
mkubwa, kuongeza uwajibikaji, moyo wa kujitolea na kutojiona kama vile mgonjwa
aliyeumia anatumiwa kama mojawapo ya kuongeza kipato kwa watendaji.
Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and
Immunology), Profesa John Shao, akizungumzia uzoefu wake katika masuala ya kuhudumia wafanyakazi waliopata madhara mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na usalama mahala pa kazi wakati wa mafunzo ya madaktari wanaojifunza namna ya kufanya tathmini
ya Mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana
na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka Kanda ya Kaskazini mjini Moshi
Februari 21, 2018
Mshiriki akifuatilia kwa makini nasaha za Profesa Shao.
Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), na Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Assessment Manager), wakifuatilia nasaha za Profesa Shao.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akiongoza mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza kufuatia mada zilizowasilishwa kwa washiriki hao. |
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza kufuatia mada zilizowasilishwa kwa washiriki hao.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia), akisalimiana na Profesa John Shao.
Profesa John Shao, akisalimiana na Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), Dkt. Ali Mtulia.
Sehemu ya washiriki.
Profesa John Shao.
Daktari bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina, akifafanua jambo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.