ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 21, 2018

VIDEO:- IMEGUNDULIKA KUWA WANAOMPINGA MKUU WA WILAYA YA KWIMBA NI WAZEMBE NA WAZURURAJI


Madiwani wa halmashauri ya wilaya kwimba mkoani Mwanza wamepinga madai kuwa mkuu wa wilaya hiyo Mhandisi Mtemi Simioni amekuwa akiwaamrisha Polisi kuwakamata baadhi ya wananchi wa kata ya Ngudu kwa kisingizio cha uzururaji na kisha kuwalimisha kwenye shamba lake.

Ni Siku mbili baada ya baadhi ya wananchi wa kata ya Ngudu wilayani kwimba mkoani Mwanza kuzuia msafara wa waziri mkuu Kasimu Majaliwa wakitaka kuondolewa kwa mkuu wa wilaya hiyo mhandisi MTEMI SEMEON kwa madai kuwaamrisha polisi kuwakamata kwa kisingizio cha uzururaji na kisha kuwalimisha kwenye shamba lake.

Kufuatia malalamiko hayo ya baadhi ya  wananchi ,Madiwani wa halmashauri ya Kwimba mkoani Mwanza ambao wamekutana na vyombo vya habari  wamesema kuwa madai hayo si ya kweli na kwamba wananchi wa ngudu waliosimamisha msafara wa waziri mkuu KASIMU MAJALIWA wanatumiwa na kikundi cha watu kisichotaka watu kufanya kazi pamoja na wale waliokuwa wakijipatia fedha za umma kwa njia za udanganyifu kabla ya mianya hiyo kuzibwa na mkuu huyo wa wilaya. 

Hawa ni baadhi ya Madiwani wa halmashauri hiyo ya Kwimba wakiongozwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Shija Malando ambao kwa pamoja wakatoa msimamo wao kuhusu kitendo cha diwani wa kata ya Gudu Juston Malifedha.

Madiwani hao ambao wamejitokeza mbele ya vyombo vya habari wakaeleza kiini cha sintofahamu iliyojitokeza katika ziara ya ya mhe.kassim majaliwa kassim.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.