Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miundo mbinu ya maji safi na maji taka iliyopo katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amemshukuru Naibu Waziri Aweso kwa msikamano ambao amekuwa akiufanya na wilaya yake ya kuwapa kipaumbele cha kuwatembelea mara kwa mara hali inayoamsha maendeleo zaidi.
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASCO, Injinia Aron Joseph amewaomba wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kwa vile kwasasa wamejipanga zaidi kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa walio pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wakati alipofanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya maji kwa jiji la Dar es Salaam ambapo amejionea maendeleo mbali mbali ya ujenzi. Pichani akiwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya alipoanzia ziara hiyo.
Akikagua mradi wa Maji Taka (DEWAT) - Mlalakuwa.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mradi wa maji eneo la Makongo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akipewa maelezo machache na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wakati Waziri Awezo alipofanya ziara ya mradi wa maji eneo la Makongo juu ambapo ujenzi bado unaendelea.
Viongozi wa DAWASA, DAWASA pamoja na uomgozi wa serikali ya kijiji wakimsikiliza Naibu Waziri Aweso.
Wakitoka kukagua mradi wa ujenzi wa makongo juu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi akisalimiana na Meneja wa DAWASCO-Kimara, Peter Fumbuka. Ambapo aliweza kumshukuru na kumpongeza kwa utendaji kazi wake na kumuomba achape kazi kwa bidii.
Muonekani wa ujenzi tanki la maji Makongo juu.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na mmoja ya wafanyakazi wa ujenzi wa mradi huo.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG- DAR.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amewataka wakandarasi walio wazembe wasipewe kazi kwa vile wamekuwa wakirudisha nyuma maendeleo kwa kuwakosesha wananchi kupata maji kwa wakati.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara katika wilaya ya Kinondoni ili kujionea ujenzi mbali mbali ya miundo mbinu inayoendeshwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na Shirika la majisafi na majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO).
Naibu Waziri Aweso amesema kuwa wakati umefika kwa wale wakandarasi wazembe kuacha kuchezea kazi wanazopewa, wafanye kazi kwa bidii ili huduma za maji zitolewe kwa wakati.
"Nawaomba sana wale wakandarasi wazembe waache kuwepewa kazi maana wanachafua wilaya ya Kinondoni na Tanzania kwa ujumla maana nimetembelea miradi mbali mbali nimejionea uzembe unaofanywa na wakandarasi, ukiangalia mkandarasi kapewa hela asilimia 70 ila kazi aliyofanya ya asilimia 40 hii haikubaliki kabisa.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amemshukuru Naibu Waziri Aweso kwa msikamano ambao amekuwa akiufanya na wilaya yake ya kuwapa kipaumbele cha kuwatembelea mara kwa mara hali inayoamsha maendeleo zaidi.
"Mimi sina mengi nitatekeleza maelekezo yote ambayo ameyatoa na nitakuwa msitari wa mbele kutoa maamuzi ya kina kwa wale makandarasi wazembe, sitamuonea aibu mtu,' amesema Naibu Waziri Aweso.
Nae Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASCO, Injinia Aron Joseph amewaomba wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kwa vile kwasasa wamejipanga zaidi kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa walio pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
"Tunamalizia ujenzi wa matanki makubwa ambayo tutaweza kuwasambazia wananchi wengi zaidi maji hasa walioko pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam," amesema Injinia Aron.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.