ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 16, 2020

Kili Canvas yawa kivutio kwa wakimbiaji Dar


Dar es Salaam Februari 15, 2020: Kili Canvas iliyozinduliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager hivi karibuni jijini Dar es Salaam, imekuwa kivutio kikubwa kwa wakimbiaji mbalimbali wa jiji hilo.

Canvas hiyo ina lengo la kuhamasisha wakimbiaji wa vitongoji tofauti vya Jiji la Dar es Salaam na Mji wa Moshi katika kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi Mosi, 2020 mkoani Kilimanjaro

Kili Canvas ni picha maalumu iliyochorwa kwa ukubwa ambapo mkimbiaji yeyote akipita karibu yake anapigwa picha na picha hiyo yenye muunganisho wa teknolojia ya kisasa baadaye kumtumia picha hiyo kupitia simu yake ya mkononi. Hata hivyo mkimbiaji anatakiwa kujisajili na kupewa chip maalumu ambayo anatakiwa kuwanayo kwa maelekezo ya wahusika.

Mtangazaji wa Wasafi Redio Fm, Maulid Kitenge mmoja wa wakimbiaji wa Wasafi Jogging Club ambye amevutiwa na Canvas hiyo jijini Dar es Salaam, alisema, “Hii ni teknolojia nzuri ambayo inakupatia picha yako tena nzuri pasipo kupata taabu yoyote. 

Binafsi napendelea sana kufanya mazoezi nikishirikiana na Wasafi Jogging kwani mazoezi ni afya lakini mazoezi humfanya mtu kuonekana mpya kila wakati na zaidi mazoezi ni sehemu ya michezo ambao umenifanya kufahamiana na marafiki wengi.
Kitenge alisema mwaka jana nilikimbia Kili Marathoni lanini mwaka huu pia lazima nishiriki pia kwa kuvuna record yangu yam waka jana.Si mimi tu bali wanafamilia wote wa Wasafi Jogging tunatarajia kushiriki Kili Marathon 2020.

Wito kwako wewe Mtanzania ambapo mashindano haya hufanyika Nchini kwako kila mwako na haushiriki,”Tuungane 2020 kama Watanzania tukashiriki kilele cha mbio za Kili Marathon pale Mkoani Kilimanjaro kwani ni takribani nchi 52 Duniani hushiriki mashindano hayo.

Nae Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli alisema kuwa, mtu yeyote anayependa mchezo wa kukimbia anaweza kupata fursa ya kupita katika Canvas hiyo na kufaidi teknolojia hiyo ya kisasa ya kupigwa picha na kasha kutumiwa katika simu yake.

“Hii ni fursa kwa kila mtu anayependelea mchezo wa kukimbia, na si lazima awe ni mshiriki wa Kili Marathon, ndiyo maana tukasema yeyote anaweza kujisajili na kupata chip hiyo kwa kipindi hiki cha kuhamasishana kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon,” alisema Kikuli. 

Kwa mujibu wa Kikuli, Canvas hiyo ilikuwa katika Ufukwe wa Coco Beach Masaki, lakini kwa siku tatu yaani Februari 17-19,2020 itakuwa Uwanja wanje wa Taifa Temeke na Februari 20 – 21,2020 Canvas itakuwa Viwanja vya Leaders na baadae kuelekea Moshi Mkoani Kilimanjaro.

 “Ili uweze kupigwa picha na kutumiwa kwenye simu yako kwa wale wakimbiaji ni lazima ujisajili na kupewa Chip maalumu ambayo utaelekezwa wapi pa kuiweka wakati unakimbia. Mara tu utakapopita karibu na Canvas kamera zetu zitakutambua na kukupiga picha kwa teknolojia maalumu na kutumiwa papo hapo kwenye simu yako” Kikuli alisema

Kwa mujibu wa Meneja huyo, usajili bado unaendelea kwaajili ya kujipatia Chip unafanyika Mlimani City na Uwanja wa Taifa Temeke pale njea jijini Dar es Salaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.