"HAIJALISHI NI KATIKA MICHUANO GANI: kombe la mbuzi, mechi za mchangani, nje ya afrika iwe bara au visiwani KISASI NI KISASI TU!!" asema PJ wa Power Breakfast.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Mapinduzi nahodha wa Simba Sc Nicco Nyagawa baada ya timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi jijini Dar kuilamba Yanga bao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika usiku wa kuamkia leo uwanja wa Amaan Stadium Zenji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein katika pozi na kikosi cha Simba kabla ya mchezo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akipozi na kikosi cha Yanga kabla ya mchezo.
Simba na Yanga katika 'eksheni'.
Simba woyeeeeeeeeee…...Mashabiki wa simba hakuna kulala!!
Dakika ya 33 Mussa Hassan ‘Mgosi’ aliipatia Simba bao la kwanza baada ya kupokea pasi safi iliyopigwa kutoka wingi ya kulia na kuachia shuti kali lililomshinda kipa Yaw Berko wa Yanga na kujaa moja kwa moja wavuni. Bao la pili lililoiwezesha Simba kuibuka na ubingwa lilifungwa na Shija Mkina.
KOICA Yajenga Maabara ya Kisasa ya 3D ATC
-
Na Woinde Shizza, Arusha
Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya
Kimataifa la Korea (KOICA), kimezindua rasmi maabara...
Simba SC inafahamu la kufanya ili 'kupindua meza'
-
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids amesema wachezaji na jopo la ufundi
wanafahamu fika wanachopaswa kukifanya katika mchezo wa marejeano wa
fainali ya Ko...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.