ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 13, 2011

Mdau ... UMESOMEKA!!..!!

Hi Sengo
hongera sana kwa kutufanya hata sisi tulio mbali na tanzania hususani mwanza kuelewa nini kinaendelea, nilikuwa na maombi yafuatayo nikiwa kama mfuatiliaji wa blog yako kila siku hata kama sicommet chochote lakini huwa lazima nifungue mara nyingi huwa najulikana kama bm.

1. kuna habari huwa unazianzisha lakini baadaye unatuacha kwenye mataa, mfano uliwahi kuandika bustani ya eden ndani ya mwanza lakini mpaka leo hatujui kama inaendelea kujengwa au mradi ulikuwa feki umekufa? uliwahi kusema machinga wataondolewa makoroboi kupisha kikwangua anga cjui ujenzi umeshaanza au vipi na ni hoteli, ofisi au shopping malls au vyote kwa mpigo na linamilikiwa na nani? ulisema ppf kuendelea kupendezesha mwanza kwa majengo, je kuna ujenzi wowote unaoendelea hapo mwanza ukiwa kama mradi wa ppf au nssf kwa sasa? ulitoa ramani ya soko mwanza je litaanza au limeshaanza kujengwa lini? rumours imevunjwa kunajengwa nini........ pamoja na mangine mengi. nafikiri ukiwa kama mwandishi wa habari unaweza hata kuongea na viongozi wa jiji wakakupa undani wa mambo yalivyo au ni wakali?

2. naweza kupata picha za chuo cha saut pamoja na maeneo mengine yanayojengwa kisasa mwanza mfano. kiseke, nyakato bwiru isamilo, nyegezi, capripoint, ilemela nk si lazima sana ila nikipata nitashukuru haina haraka sana hata kama itapita miezi kadhaa maana najua na wewe uko busy na hii ya blog unajitolea tu. hizo picha ni wewe mwenyewe uzpost au unitumie kwenye email kwangu vyovyote poa tu.

pole kwa maelezo mengi na ahsante kwa kazi unayofanya Mungu akubariki wewe na familia yako.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.