Tamko hilo linaonekana kukinzana na lile la ruksa ya kuendelea kufanya biashara toka kwa Mbunge wa Nyamagana Ezekia Wenje (Chadema) alilolitoa siku chache zilizopita wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kulaani tukio la polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa Chadema Arusha katika mkutano uliofanyika viwanja vya Ngoko’s vilivyopo Kata ya Milongo jijini mwanza.
Meya Manyerere amefafanua kuwa kutokana na hadhi ya Jiji la Mwanza na kusifika kushika nafasi ya kwanza ya usafi kwa miaka mitano mfululizo, likitembelewa na wageni mbalimbali wa kitaifa na kimataifa ili kuilinda hadhi hiyo uongozi hawana budi kuwaondoa wamachinga na mama ntilie ambao wamekuwa kero na kusababisha kuziba barabara za watembea kwa miguu sambamba na kuacha uchafu kila maeneo.
Meya Amewataka wabunge na madiwani wa Jiji la Mwanza kuacha tabia ya kuwapotosha wananchi na badala yake wawe mstari wa mbele kuwaeleza ukweli na kuwaweka tayari kufuata taratibu na sheria zilizopo ili jiji la mwanza liendelee kuwa kioo katika suala la usafi na utunzaji mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza bw. Wilson Kabwe amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia kanuni na sheria kwa kuondoka maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara na kuelekea kwenye maeneo waliyopangiwa toka awali.
Maeneo yaliyotengwa kwaajili ya wafanyabiashara hao ni Kiloleli, Buzuruga, Kitangili, Nyegezi, Mlango mmoja, Mabatini na kwenye magulio katika maeneo ya Mkuyuni, Igombe, Sabasaba, Nyakato National, Kayenze, Kitangiri, Buhongwa, Mkolani, Igogo, Magomeni Kirumba na Igoma hii ni kwa kufuata siku kama ilivyopangwa na si vinginevyo.
Tupe maoni yako
kweli jiji lisafishwe
ReplyDeleteJamani napenda kuuliza huyu meya anawalinda kweli au anawapenda wamachinga?anaonesha anataka kuwarudisha vijijini wakalime hiyo ndiyo sera ya chadema.
ReplyDelete