ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 10, 2011

WANAHABARI WALIPOTEMBELEA TBL.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kiwanda chake kilichopo ilemela jijini Mwanza mwishoni mwa wiki ilitoa fursa kwa waandishi wa habari kutembelea kiwanda hicho kwa nia ya kujionea utayarishwaji na utengenezwaji wa vinywaji vyake.

Wanahabari wa walipata maelezo ya kina, hatua kwa hatua huku nao wakiuliza maswali mengi, mengi kama vile nao wanakwenda kuwa wajasiliamali kwa kuanzisha viwanda vyao.

Production juu kwa juu kiwandani hapo, Teknolojia ina athari zake imajin mitambo yote hii yajiendesha kwa mfumo wa kompyuta ikisimamiwa na watu watatu wanne...hivi.

Mitungi ya kupikia kileo aka 'gambe' aka 'bata'.

Teknolojia ya kisasa katika uchanganyaji na upikaji ikielekeza mwonekano toka kwenye mitungi.

Ubebaji wa kinywaji kilicho kamilika kutoka kiwandani hatimaye kuingia sokoni.

Utoaji chupa kwenye masanduku kwaajili ya hatua ya uoshaji.

Chupa husafishwa kwa kutumia maji yenye joto la hali ya juu lenye uwezo wa kuondosha taka za aina zote.

Utengenezwaji wa kinywaji kipya cha kiasili NZAGAMBA, kinacho tengenezwa kwa teknolojia ya kisasa.

Shughuli za kutembelea kiwanda zilipo kamilika 'MIMINAMIMINA TIME' ikawadia, ikiwa ni pamoja na wanahabari kushindanishwa katika zoezi la kutambua vinywaji kupitia ladha, rangi na mengineyo. Zawadi za nguvu zilitolewa kwa washindi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.