
Matokeo mabaya yameifanya Liverpool kuteremka hadi nafasi ya 12 katika ligi kuu ya Premier. Mchezaji wa zamani na vile vile meneja, Kenny Dalglish, atashikilia madaraka ya meneja hadi mwisho wa msimu.
"Pande zote mbili ziliafikiana kwamba kwa kuzingatia maslahi yao, ni vyema aondoke", alielezea Mmarekani anayemiliki klabu, John W Henry, kupitia maelezo katika tovuti ya klabu.

Wakati mkutano wa Liverpool kuzungumza na waandishi ulipofutiliwa mbali siku ya Ijumaa, kuzungumzia juu ya mechi ya Jumapili ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United, uvumi ulizuka mara moja kwamba mkataba wa kocha huyo ambaye zamani aliiongoza Fulham, ulikuwa hatarini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.