Rais wa Sudan Omar al-Bashir ameonya kwamba Sudan Kusini haitokuwa tulivu ikiamua kupiga kura ya kujitenga na kaskazini katika kura za maoni.RAIS WA SUDAN OMAR BASHIR & KIONGOZI WA KUSINI SALVA KIIR. Aliiambia televisheni ya al-Jazeera kuwa kusini haina uwezo wa kuunda taifa thabit au kuwahudumia wananchi wake. Mwandishi wa BBC James Copnall mjini Khartoum alisema kauli hiyo itawakera sana waliokuwa waasi wa SPLM ambao wamekuwa wakiiongoza kusini tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika mwaka 2005. Mikutano ya mwisho imekuwa ikifanyika upande wa kusini kabla ya kura kuanza siku ya leo (Jumapili).
Waandishi wanatarajia kura ya “ndio” kwa kishindo, itakayo sababisha kuzaliwa kwa nchi nyingine duniani. Kura hii ya maoni ni sehemu ya makubaliano ya mwaka 2005 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo miwili baina ya kaskazini na kusini.
UCHAGUZI 2025: BALOZI NCHIMBI ATOA WITO
-
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
amesema kuwa msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu
pamoja na...
UCHAGUZI 2025: BALOZI NCHIMBI ATOA WITO
-
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
amesema kuwa msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu
pamoja na...
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.