Japo kwa uchache familia yetu.
Brother Adam mbele ya kaburi la babu yetu Mzee Sospeter, kaburi lililopo hatua chache toka kaburi la marehemu baba.
Watoto wanapenda sana kujifunza kwa kuuliza maswali tena mengi ya kudadisi, hili nililiona kwa mtoto huyu wa braza ambaye nae aliomba kupiga picha ya kumbukumbu.
Hazina za kwetu milima ya mawe.
Wakati wa umiliki wa eneo hili kupitia Tajiri mmoja aliyekuwa mwekezaji wa magari yaliyokuwa na chata 'REHEMA YA MUNGU' namzungumzia Paul Ng'wani, Kituo hiki cha mafuta kilikuwa kinang'aa kisawasawa yaani hapa ndiyo penyewe, town centre babaake!.
Aya-ya-yaaa Fagia sana kiwanja hapo mbele... 'Home sweet home' nyumbani kwa Mzee Kaseko.
George na Nduguye mpya katika pozi.
Hiki ni moja kati ya kitaa kilicho shiriki kunikuza (just for three years). "Kiukweli kama neema imepotea hivi tofauti" nakumbuka Enzi hizo nyumba zilikuwa smati na hata kama za udongo zilinakshiwa na chokaa huku watu wakishindana kupanda maua mbele ya nyumba yaani full green. Lakini sasa MMMMh!
Tupe maoni yako
mji gani huu Albert,safi sana kwa kukumbuka nyumbani,na pole pia kwa kumpoteza mzee
ReplyDelete