Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja anadaiwa kuua watoto wake wawili, Kumchoma visu mume wake mara tatu kabla ya kujaribu kujiua eneo la Ongata Rongai.
Mwanamke huyo ambaye amelazwa katika Hospitali Kuu
ya Kenyatta na akiwa hali mahututi, anasemekana kumchoma visu mume wake kufuatia ugomvi katika nyumba yao
kwenye barabara ya Maasai Lodge.
Ugomvi huo ulielekea pabaya baada ya mwanamke huyo
kumdunga mume wake mara tatu – kichwani,shingoni - baada yake kurejea nyumbani
saa saba usiku, polisi wanasema.
Mwanamume huyo alinusurika kifo baada ya kukimbia
kutoka kwa nyumba hiyo akibubujikwa na damu na kuomba msaada kutoka kwa
majirani ambao walimkimbiza kwenye kituo cha afya kilicho karibu
Kwa mujibu wa polisi, mama huyo wa watoto wawili
ambaye alibaki nyumbani, anasemekana kufunga milango kabla ya kuua wanawe wawili
- miaka sita na miwili – kuwachoma visu.
Polisi wanasema kuwa alijaribu kujiua kwa kisu hicho
lakini juhudi zake ziliambulia patupu.
Alisalia na
vidonda kwenye tumbo na kifua.
Polisi waliitwa eneo la tukio na kupeleka miili hiyo
kwenye hifadhi ya maiti.
Wanandao hao wamelazwa hospitalini chini ya ulinzi
mkali. Kamanda wa Polisi wa Kajiado Kaskazini Hussein Gura alisema kuwa polisi
walipata silaha iliyoyumiwa kutekeleza mauaji hayo na wameanzisha uchunguzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.