ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 9, 2023

MKOA WA PWANI WASHUSHA KIKOSI CHA WACHEZAJI 120 MICHUANO YA UMISETA TAIFA

 


Na Victor Masangu,Pwani 


Jumla ya wachezaji wapatao 120 wamechaguliwa kwa ajili ya kuunda kikosi cha timu ya Mkoa wa Pwani kitakachoshiriki katika mashindano ya Umoja wa michezo na sanaa kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya Taifa itakayoanza kutimua vumbi Juni 15 hadi 25 mwaka huu  mkoani Tabora.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Buleta amesema kwamba wachezaji hao wamechaguliwa kutokana na uwezo na vipaji walivyonavyo  katika fani ya michezo mbali mbali.

Buleta alitasema hayo wakati wa halfa ya kutangzwa kwa kikosi cha wachezaji iliyofanyika katika viwanja vya shirikika la elimu Kibaha na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo walimu,Wanafunzi pamoja na wadau wa michezo.

Afisa michezo huyo alisema kwamba wachezaji hao wataingia kambini kwa kipindi cha muda wa siku tano kwa ajili ya kujiandaa na kujinoa vilivyo kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mashindano ya Kitaifa mkoani Tabora tarehe 14 mwezi huu.


"Tunashukuru tulikuwa na wachezaji wapatao 700 hapo awali lakini baada ya kufanya mchujo tumefanikiwa kupata wachezaji wapatao 120 ambao ndio watakaouwakilisha Mkoa wa Pwani katika mashindano ya  Taifa mkoani Tabora,"alisema Buleta.

Kadhalika aliongeza kuwa katika mashindano ya mwaka huu wachezaji wamejipanga vilivyo kuweza  kuibuka na ubingwa  wa Kitaifa kutoka na kujiandaa vizuri katika michezo mbali mbali watakayoshiriki.

Amebainisha michezo ambayo watashiriki katika michuano hiyo ni pamoja na Netiboli,mpira wa miguu,kikapu,wavu,mpira wa mikono,riadha,fani za ndani,ngoma,kwaya sambamba na mziki wa kizazi kipya.

Katika hatua nyingine alimshukuru kwa dhati mdau wa michezo ambaye pia ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Mussa Mansoor kwa kuchangia vifaa mbali mbali vya michezo kwa timu ya Mkoa ili iweze kufanya vizuri.

Kwa upande wake Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Mussa Mansoor alisema lengo lake kubwa ni kusaidia kukuza sekta ya michezo kuanzia ngazi za chini kwani michezo kwa sasa ni fursa za ajira.


Pia aliongeza kuwa ametoa vifaa mbali mbali vya michezo kwa lengo la kuwasaidia vijana waweze kupata fursa ya kuonyesha na kuibua vipaji vyao walivyonavyo.

 Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo amewataka wanamichezo ambao wamechaguliwa kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ili waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo ngazi ya Taifa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.