ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 5, 2011

ZAIDI YA AKINAMAMA 30 WAPEWA ELIMU YA USINDIKAJI SABUNI

Jumla ya akina mama wawakilishi kutoka vikundi mbalimbali wapatao 30 wa Kata ya Mbugani wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wamenufaika na mafunzo ya ujasiliamali ya kutengeneza sabuni kwaajili ya kuanzisha viwanda vidogovidogo vitakavyo wasaidia kuongeza kipato na kujikwamua kiuchumi. Diwani wa viti maalum jimbo la Nyamagana Bi Neema Mafuma akitoa maelezo kwa washiriki namna ya kusindika sabuni.

Mafunzo hayo ya siku tatu yametolewa na wawezeshaji kutoka Mfuko wa Mbunge wa Wilaya ya Nyamagana mh. Ezekiel Wenje , chini ya usimamizi wa diwani wa viti maalum jimbo la Nyamagana kata ya Mahina bi. Neema Mafuma kwa lengo la kuwafundisha mbinu zaidi za ujasiliamali kwaajili ya kujipanua kwenye soko la uzalishaji mali hasa kwa bidhaa zinazohitajika sokoni.

Mpango huo umetoa elimu kwa akina mama hao ili kukabiliana na mfumuko wa bei unao likabili taifa hasa kwa bidhaa za matumizi ya kila siku ambapo nyingine zinaweza kutengenezwa na vikundi vidogo vidogo hivyo kupunguza makali ya maisha kwa kuuzwa kwa bei nafuu kwa jamii.





Tupe maoni yako

2 comments:

  1. wanawake na maendeleo poa sana

    ReplyDelete
  2. mimi niko SAUT chuoni, ninaomba contacts za mh.diwan wa mafunzo ya sabun, ninahtaji kupata maelekezo zaidi ya jinsi ya utengenezaji wa sabuni. Niko chuon ila nafanya mradimdogo wa kutengeneza sabun zakigoma.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.