



Wananchi hao ambao walikuwa na shauku ya kuuaga mwili wa marehemu huyo walijitokeza kwa wingi huku wakionekana kuwa na nyuso za majonzi, kila mmoja akihuzunika na wengi wakidai kuwa mwimbaji huyo wa bongo flava ameacha pigo kubwa kwa jamii ya kimasai na Taifa kwa ujumla kwani muziki wake sambamba na kuburudisha ulikuwa unaelimisha kwa kiwango kikubwa.
Akiongea katika mazishi hayo askofu mkuu wa jimbo la kaskazini Thomas Laizer alisema kuwa wao kama kanisa wameupokea msiba huo kwa masikitikio makubwa kwani msanii huyo alikuwa anaelimisha jamii kupitia nyimbo zake pia aliweza kuutangaza mkoa wa Arusha pamoja na thaminisha asili ya kabila la kimasai kupitia nyimbo zake.
Tupe maoni yako
inalillah wainalilahh rajeun
ReplyDeleteI am a LUO who grew up as a Bantu Tribe, My Identity was Changed, I personally will miss Ebbo; Education and fun..The only 1 we had.. Yusuf Musoke..Uganda
ReplyDelete