Hayo yamebainishwa naye Kaimu M/kiti wa chama cha basketball mkoa wa Mwanza Sosho Kizito, wakati akipokea msaada wa seti moja ya jezi toka kwa uongozi wa Klabu ya Burudani ya Rock Bottom ya jijini Mwanza.
Sosho amesema kuwa kutokana na timu hizo kuwa na mahitaji mbalimbali kama vile gharama za kambi, usafiri, chakula na malazi, huku kukiwa hakuna dalili yoyote kwa timu zake kupata mafungu ya uwezeshwaji Chama cha mpira wa kikapu Mkoa wa Mwanza kimeamua kupeleka timu moja tu kwenye mashindano hayo ili angalau kuweza kuepuka aibu ya kukosa kushiriki kabisa.
Ben Mwangi.
Kwa upande wake Consolting Manager wa Gold Crest Hotel Ben Mwangi amesema kuwa Club yake imetoa msaada huo mara baada ya kuona hali ngumu inayoikabili timu hiyo, hivyo anaamini kabisa kuwa msaada huo utatumika kutia hamasa kwa Wanamwanza kujitokeza katika kufanikisha ushiriki wa timu yao.
Taarifa zinasema kuwa bado milango ya kupokea ufadhili iko wazi kwa wale wote wenye mapenzi mema na mafanikio ya Mwanza katika michezo.
Ili timu ya mkoa wa Mwanza wanaume kwa wanawake ziweze kushiriki vyema kwenye mashindano hayo kiasi cha shilingi milioni 10 kinahitajika.
Timu ya wanaume inaundwa na wachezaji wafuatao:- John Sapa Pastory, Eric John, Paschal Imanyi Magabe, Innocent, Ernest Masanja (Bugando Worrious), Victor Zacharia, Amran sufian, Bundala Charles, Simon Chelu, Timothy Ngalula (Bugando Heat), Evordius Henga, Vincent Shinda, Enock Charles, Samwel Mujanja, Ally Issa (Butimba Spider), Ahmed Said, Amri Mohamed (Dolphins Pasiansi), Amon Semberya, Francis Shilinde, Wilson Masanja na Kiziti Sosho Bahati (Bugando Planet), wachezaji walio nje ya mkoa wa mwanza ni pamoja na Adam Jegame, Juma kissoky na Mohamed Ally Dibo. Timu hiyo ipo chini ya kocha Robert John Mwita.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.